WENYEJI, Pamba Jiji FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Namungo FC walianza kupata bao dakika ya 22 likifungwa na kiungo mkongwe, Jacob Raymond Masawe, kabla ya mshambuliaji Mguinea, Abdoulaye Yonta Camara anayecheza kwa mkopo kutoka Singida Black Stars kuisawazishia Pamba Jiji FC dakika ya 34.
Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji FC inafikisha pointi 23, ingawa inabaki nafasi ya 13 ikizidiwa pointi moja na Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 24.
0 comments:
Post a Comment