Tuesday, April 08, 2025

    PAMBA JIJI NA FOUNTAIN GATE HAKUNA MBABE, 1-1 KIRUMBA


    WENYEJI, Pamba Jiji FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Pamba Jiji walianza kupata bao kwa penalti likifungwa na mshambuliaji Mkenya,  Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 22, kabla ya kiungo Mrundi mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Elie Eldhino Mokono kuisawazishia Fountain Gate dakika ya 61.
    Pamba Jiji FC watajilaumu wenyewe kwa kutoondolka na pointi zote za mchezo wa leo baada ya Methiw Tegisi kukosa penalti dakika ya 90+7.
    Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya 10, huku Fountain Gate ikifikisha pointi 29 na inabaki nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA JIJI NA FOUNTAIN GATE HAKUNA MBABE, 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry