TIMU ya Singida Black Stars imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Niger,
Adebayor Zakari Victorien Adje dakika ya 11 na mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 66.
Kwa ushindi huo Singida Black Stars itakutana na Simba SC katika Nusu Fainali ambayo iliitoa Mbeya City jana kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment