• HABARI MPYA

        Friday, April 11, 2025

        MMILIKI WA MAN UNITED AKABIDHIWA JEZI YA YANGA


        MMILIKI mwenza wa klabu ya Manchester United ya England, Sir. Jim Ratcliffe leo amekabidhiwa jezi ya klabu bingwa ya Tanzania, Yanga SC yenye jina lake.
        Sir. Jim Ratcliffe anayemiliki asilimia 28.94 katika klabu ya Manchester United dhidi ya asilimia 71.06 za Malcolm Glazer na Familia yake — amekabidhiwa jezi hiyo Jijini Far es Salaam na Rais wa Yanga,  Hersi Said walipokutana.
        Sir Ratcliffe, mmiliki wa taasisi ya Six Rivers Africa inayosaidia miundombinu, tafiti na uendelezaji wa uhifadhi na utalii — yupo nchini kwa mwaliko wa Serikali na leo amekutana na Rais wa Yanga, Hersi ambaye pia ni
        Mwenyekiti wa Umoja wa klabu Afrika (ACA) na kujadili mambo machache ikiwemo kuhusu utalii na michezo. 
        Yanga imeahidi kushiriki kwa nafasi kubwa katika kutangaza na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sera yake kubwa ya utalii. 

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MMILIKI WA MAN UNITED AKABIDHIWA JEZI YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry