Thursday, April 10, 2025

    MASHUJAA FC YAIKUNG’UTA TABORA UNITED 3-0 KIGOMA


    WENYEJI, Mashujaa FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Mundhir Abdullah Vuai dakika ya nane, Jaffar Salum Kibaya dakika ya 45’+5 na David Richard Ulomi dakika ya 87.
    Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 30 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 37 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA FC YAIKUNG’UTA TABORA UNITED 3-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry