NAHODHA na Kocha wa zamani wa timu ya ya Nigeria, Christian Chukwuemeka Chukwu amefariki dunia jana (Aprili 12, 2025) akiwa ana umri wa miaka 74.
Chukwu aliyejulikana kwa jina la utani, ‘Mwenyekiti’ alizaliwa Januari 4, mwaka 1951 na kisoka aliibukia Ngwo Park — ambako kipaji chake kilimfanya avume Enugu yote.
Safari yake rasmi ya soka ilianzia klabu ya Rangers International FC ya huko huko Enugu, ambako alikuwa mchezaji tegemeo miaka ya 1970.
![]() |
|
Akifahamika kwa uhodari wake wa kuiongoza safu ya ulinzi kama beki kiongozi wa kati — alipewa jina Mwenyekiti na hiyo ilimfunfulia milango kwenye kikosi cha timu ya taifa wakati huo ikijulikana kama Green Eagles.
Mafanikio ya kwanza ya Chukwu yalikuja mwaka 1980 alipoiongoza Green Eagles kutwaa taji la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika to (AFCON) nyumbani.
Walianza kwa kuongoza Kundi A, wakishinda mechi mbili, dhidi ya Tanzania 3-1 na Misri 1-0, nyingine wako Toa sare ya 0-0 na Ivory Coast, kabla ya kwenda kuifunga Morocco 1-0 katika Nusu Fainali na kutwaa Kombe kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Algeria kwenye Fainali
Katika kipindi cha miaka nane ya utumishi wake Green Eagles kuanzia mwaka 1974 hadi 1981 alicheza jumla ya mechi 54 na japokuwa alikuwa mlinzi alifunga mabao matano.
Baada ya kustaafu soka alifundisha klabu ya Enugu Rangers mara tatu, 1982 hadi 1985, 1986 hadi 1988 na 2005 hadi 2009 pamoja na timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya miaka 17 kati ya 1985 na 1986, timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ kuanzia 1998 hadi 2003 na Super Eagles kuanzia mwaka 2003 hadi 2005.
Mungu ampumzishe kwa amani Kapteni Chukwu.
0 comments:
Post a Comment