• HABARI MPYA

        Tuesday, April 08, 2025

        KHALID AUCHO KUWAKOSA AZAM FC NA ATAKUWA NJE WIKI TATU


        KIUNGO wa Yanga, Khalid Aucho atakuwa nje kwa wiki tatu baada ya jana kuumia nyama za paja wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
        Taarifa ya Yanga jioni hii imesema kwamba Aucho amefanyiwa vipimo leo katika hospitali ya Saifee, Dar es Salaam na kugundulika maumivu hayo yatamuweka nje kwa muda huo - maana yake atakosekana kuanzia mchezo ujao dhidi ya Azam FC keshokutwa.
        Aucho aliumia mwishoni mwa kipindi cha kwanza jana baada ya kuchezewa rafu na kiungo wa Coastal Union, Lucas Almeida Kikoti na pamoja na kujaribu kujitahidi kuendelea na mchezo lakini hakumaliza kipindi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Mudathir Yahya Abbas baadaye kipindi cha pili.
        Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo huo, bao pekee la kiungo Muivory Coast Peadoh Pacome Zouzoua dakika ya 35.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: KHALID AUCHO KUWAKOSA AZAM FC NA ATAKUWA NJE WIKI TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry