WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Beki Ally Ayoub Msangi alijifunga dakika ya 59 kuipatia bao la kuongoza Kagera Sugar, kabla ya kiungo Lucas Almeida Kikoti kuisawazishia Coastal Union dakika ya 84.
Shujaa wa Kagera Sugar leo ni beki Mohamed Mussa Salum ‘Jecha’ aliyeifungia bao la ushindi timu hiyo dakika ya 90’+4.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya 14 ikizidiwa pointi moja na jirani zao, Pamba Jiji FC ya Mwanza baada ya wote kucheza mechi 24.
Kwa upande wao Coastal Union baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 25 za mechi 24 pia nafasi ya 10 kwenye Ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment