Monday, April 14, 2025

    JKT TANZANIA YAITANGULIA YANGA FAINALI KOMBE LA CRDB


    TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Pamba Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Yunus Lema aliyejifunga dakika ya 36 na Mohamed Bakari mawili dakika ya 74 na 85, wakati bao pekee la Pamba Jiji limefungwa na Henry Msabila dakika ya 90’+3.
    JKT Tanzania itasubiri mshindi wa kesho baina ya mabingwa watetezi, Yanga na Stand United kwa ajili ya Nusu Fainali ya michuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAITANGULIA YANGA FAINALI KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry