• HABARI MPYA

        Friday, April 11, 2025

        JKT TANZANIA NA NAMUNGO HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI


        TIMU ya JKT Tanzania imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Alhamisi Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
        Mabao ya JKT Tanzania yalifungwa na viungo, Maka Edward Mwasomola dakika ya 63 na Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 69, wakati ya Namungo FC yamefungwa na kiungo pia, Salehe Kalabaka Kikuya dakika ya 18 na mshambuliaji Mkongo, Fabrice Ngoy wa Ngoy dakika ya 49.
        Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 25, ingawa inabaki nafasi ya saba — wakati Namungo FC inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: JKT TANZANIA NA NAMUNGO HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry