// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JKT TANZANIA NA DODOMA JIJI HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JKT TANZANIA NA DODOMA JIJI HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Thursday, April 03, 2025

    JKT TANZANIA NA DODOMA JIJI HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI


    WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya JKT Tanzania yote yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Edward Songo dakika ya 25 kwa penalti na dakika ya 67, wakati ya Dodoma Jiji yamefungwa na kiungo Mwana Kibuta David dakika ya 45'+2 na mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 81.
    Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 31 na wanabaki nafasi ya sita, wakati Dodoma Jiji inafikisha pointi 28 na inabaki nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi 24.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA NA DODOMA JIJI HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry