Wednesday, April 09, 2025

    DODOMA JIJI YAITWANGA KAGERA SUGAR 2-0 JAMHURI


    WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na winga Iddi Bahati Kipagwile kwa penalti dakika ya 37 kwa penalti na mshambuliaji Hassan Omary Mwaterema dakika ya 85.
    Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 34 na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 22 nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAITWANGA KAGERA SUGAR 2-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry