TIMU ya Stand United imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Giraffe Academy leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mabao ya Stand United yamefungwa na Khalid Jaffary dakika ya 59, Msenda Senga dakika ya 70 na Omary Ramadhani dakika ya 84, wakati bao pekee la Giraffe Academy limefumgwa na Zelfin Malima dakika ya 73.
0 comments:
Post a Comment