Tuesday, March 11, 2025

    PRINCE DUBE MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI, HAMDI KOCHA BORA


    KLABU ya Yanga imeshinda Tuzo za Kocha Bora na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Februari mwaka huu.
    Mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo amewashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki na mshambuliaji wa Kengold, Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' kutwaa Tuzo hiyo.
    Kwa upande wake Kocha Mualgeria wa Yanga, Miloud Hamdi amewashinda Muafrika Kusini, Fadlu Davids wa Simba na mzawa, Freddy Felix Minziro wa Pamba Jiji.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PRINCE DUBE MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI, HAMDI KOCHA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry