REFA Ahmed Arajiga ndiye atakayepuliza kipyenga kwenye mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Yanga na Simba Jumamosi wiki hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Arajiga, Refa Bora wa nchi katika mchezo atasaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam watakaokuwa wakikimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja, wakati mezani atakuwepo Amina Kyando wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment