MCHEZO wa kirafiki baina ya wenyeji, Singida Black Stars na Yanga ya Dar es Salaam imechezwa kwa dakika 57 tu, kabla ya kusitishwa kutokana na mvua kali iliyokuwa inanyesha Uwanja wa Airtel mjini Singida.
Hadi mchezo huo unasitishwa timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia na bao la winga Mkongo, Jonathan Ikangalombo dakika ya 19, kabla ya kiungo Mtogo, Marouf Tchakei kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 55.
Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa maalum kuuzindua Uwanja wa huo mpya wa Airtel uliopo eneo la Mtipa ambao utakuwa wa nyumbani wa Singida Black Stars ambayo awali ilikuwa inatumia Uwanja wa CCM LITI uliopo Singida mjini.
Yanga wanaweza kurejea Dar es Salaam kesho kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB dhidi ya Songea United Jumamosi Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge.
0 comments:
Post a Comment