WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao yote ya Azam FC leo yamefungwa na wazawa, kiungo mshambuliaji Nassor Saadun Hamoud dakika ya tano na mabeki, Pascal Gaudence Msindo, mawili dakika ya 45’+2 na 57 na Lusajo Elukaga Mwaikenda dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 48, ingawa inabaki nafasi ya tatu na Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 18, nayo inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 23.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment