Thursday, March 06, 2025

    MOKONO APIGA ZOTE MBILI FOUNTAIN GATE YAICHAPA KMC 2-1 MWENGE


    TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo Mrundi mzaliwa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Elie Mokono dakika ya 77 na 90’+4, wakati la KMC limefungwa na Oscar Paul kwa penalti dakika ya 45.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate wanafikisha pointi 28 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya sita, wakati KMC wanabaki na pointi zao 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOKONO APIGA ZOTE MBILI FOUNTAIN GATE YAICHAPA KMC 2-1 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry