Wednesday, March 12, 2025

    MAXI APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-1 KOMBE LA CRDB


    MABINGWA watetezi, Yanga  wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli, mawili dakika ya pili na 15, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Clement Francis Mzize kufunga la tatu dakika ya 21, wakati bao pekee la Coastal Union limefungwa na Miraj Abdallah dakika ya 18.
    Yanga sasa itakutana na Songea United iliyotoa Polisi Tanzania kwa kuichapa bao 1-0 Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXI APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-1 KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry