// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIBU NA AHOUA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI, SIMBA YAITANDIKA DODOMA JIJI 6-0 MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIBU NA AHOUA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI, SIMBA YAITANDIKA DODOMA JIJI 6-0 MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Friday, March 14, 2025

    KIBU NA AHOUA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI, SIMBA YAITANDIKA DODOMA JIJI 6-0 MWENGE


    TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo a Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala dakika ya 16, kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 21 na 45’+1, mshambuliaji Mganda, Steven  Dese Mukwala dakika ya 46 na kiungo Mtanzania mwenye asili ya Kongo, Kibu Dennis Prosper mawili pia, dakika ya 54 na 69.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57, ingawa 
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 22, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 27 za mechi 23 sasa nafasi ya nane. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIBU NA AHOUA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI, SIMBA YAITANDIKA DODOMA JIJI 6-0 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry