// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KENGOLD YATOA SARE 2-2 NA MASHUJAA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KENGOLD YATOA SARE 2-2 NA MASHUJAA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Wednesday, March 05, 2025

    KENGOLD YATOA SARE 2-2 NA MASHUJAA SOKOINE


    WENYEJI, Kengold wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Kengold yamefungwa na Yusuph Dunia aliyejifunga dakika ya 26 na Mishamo Daudi dakika y 47, wakati na Mashujaa yamefungwa na Jaffar Kibaya dakika ya 21 na Ally Nasor ‘Ufudu’ dakika ya 51.
    Kwa matokeo hayo, Kengold wanafikisha pointi pointi 16 na wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16, wakati Mashujaa inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 23.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KENGOLD YATOA SARE 2-2 NA MASHUJAA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry