TIMU ya Kagera Sugar imefanikiwa kutinga Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa penalti 5-3 dhidi ya wenyeji, Tabora United kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Katika dakika 90 za mchezo huo, Tabora United ilitangulia kwa bao la beki wake Mkongo, Andy Bikoko dakika ya tatu, kabla ya kiungo mzawa, Joseph Mahundi kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 28.
0 comments:
Post a Comment