Friday, March 07, 2025

    KAGERA SUGAR YAICHAPA PAMBA JIJI 2-1 KAITABA


    WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na kiungo Mkenya,  Shaphan Oyugi Siwa dakika ya 42 na mshambuliaji Mganda, Peter Lwasa dakika ya 63, wakati bao pekee la Pamba Jiji limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 17.
    Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 14, ikizidiwa pointi tatu na Pamba iliyopo nafasi ya 13 katika ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA PAMBA JIJI 2-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry