Friday, March 07, 2025

    JKT TANZANIA YAWAPIGA TABORA UNITED 2-1 PALE PALE MWINYI


    TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
    Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na viungo Ally Hussein Msengi dakika ya 32 na Najim Magulu dakika ya 75, wakati la Tabora United limefungwa na winga Offen Francis Chikola dakika ya 64.
    Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 30 na kurejea nafasi ya sita, ikizidiwa pointi saba na Tabora United wanaobaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAWAPIGA TABORA UNITED 2-1 PALE PALE MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry