• HABARI MPYA

        Friday, March 07, 2025

        DODOMA JIJI NA COASTAL UNION HAKUNA MBABE, ZATOKA SULUHU JAMHURI


        TIMU za Dodoma Jiji na Coastal Union ya Tanga zimegawana pointi baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
        Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 22, ikiendelea kukamata nafasi ya nane kwa kuizidi pointi mbili Coastal Union ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: DODOMA JIJI NA COASTAL UNION HAKUNA MBABE, ZATOKA SULUHU JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry