MABINGWA watetezi, Yanga wamelazimishwa sare ya bila mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 18 na kuendelea kuongoza LIgi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Simba, ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 18 pia na kusogea nafasi ya nane.
0 comments:
Post a Comment