MABINGWA watetezi, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na washambuliaji tegemeo, mzawa Clement Francis Mzize dakika ya 14 na Mzimbabwe, Prince Dube Mpumeleo dakika ya 43, wakati bao la Singida Black Stars limefungwa na mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 90’+2.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 52 katika mchezo wa 20 na kuendela kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano Zaidi ya watani wao, Simba SC ambao pia wana mechi mbili mkononi, wakati Singida Black Stars wanabaki na pointi zao 37 za mechi 20, nyuma ya Azam FC yenye pointi 42 za mechi 19.
0 comments:
Post a Comment