// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TWIGA STARS YAITOA EQUTORIAL GUINEA, SASA KUIVAA ETHIOPIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TWIGA STARS YAITOA EQUTORIAL GUINEA, SASA KUIVAA ETHIOPIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Thursday, February 27, 2025

        TWIGA STARS YAITOA EQUTORIAL GUINEA, SASA KUIVAA ETHIOPIA


        TIMU ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars imefanikiwa kusonga mbeke katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwnaia tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, (WAFCON) 2026.
        Hiyo ni baada ya sare ya 1-1 na wenyeji, Equtorial Guinea katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kufuzu  WAFCON 2026 Uwanja wa Malabo mjini Malabo.
        Twiga Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia ushindi wa mabao 3-1 kwenye  mchezo wa kwanza Alhamisi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
        Twiga Stars sasa itakutana na Ethiopia iliyoitoa Uganda kwa penalti 2-0 jana Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa kufuatia ushindi wa 2-0 uliofanya sare ya jumla ya 2-2 baada ya wao pia kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Hamz, Nakivubo Jijini Kampala.
        Tayari Twiga Stars wana tiketi ya kushiriki Fainali za baadaye mwaka huu za WAFCON, ambazo zitafanyika nchini Morocco pia kuanzia Julai 5 hadi 26.
        Kihistoria Twiga Stars imewahi kushiriki Fainali za Afrika mara moja tum waka 2010 nchini Afrika Kusini, ambako ilipiteza mechi zake zote za Kundi A, ikifungwa na wenyeji, Banyana Banyana 2-1, na Mali 3-2 na Nigeria 3-0.  
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TWIGA STARS YAITOA EQUTORIAL GUINEA, SASA KUIVAA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry