TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Equtorial Guinea katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, (WAFCON) 2026 jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na kiungo, Stumai Abdallah Athumani wa JKT Queens dakika ya 49 na washambuliaji Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ wa Mazatlán ya Mexico dakika ya 55 na Diana Lucas Msewa wa Trabzonspor ya Uturuki dakika ya 90’+4.
Bao pekee la Equtorial Guinea limefungwa na beki, Gertrudis Engueme Obiang Midje wa anayechezea klabu ya Real Sociedad II ya Hispania.
Timu hizo zitarudiana Februari 26 Uwanja wa Malabo, Malabo kuanzia Saa 10:00 na mshindi wa jumla atakutana na Uganda na Ethiopia kuwania kufuzu raundi ya mwisho ya mchujo.
0 comments:
Post a Comment