WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Beki Mnigeria, Emmanuel Ugochucku Chigozie alianza kujifunga dakika ya 67 kuiipatia Tanzania Prisons bao la kuongoza, kabla ya Emmanuel Samuel kuisawazishia Tabora United dakika ya 82.
Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 14, wakati Tabora United inafikisha pointi 34, nayo inabaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 21.
0 comments:
Post a Comment