WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Beno Khalfan Ngassa dakika ya tatu na Meshack Abraham Mwamita dakika ya 85, wakati bao pekee la Mashujaa limefungwa na Seif Abdallah Karihe kwa penalti dakika ya 31.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya 13 na Mashujaa inabaki na pointi zake 19 za mechi 17 pia nafasi ya saba.
0 comments:
Post a Comment