TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabao ya Tabora United yamefungwa na mshambuliaji Offen Francis Chikola dakika ya 52 na beki Mkongo, Andy Bikoko dakika ya 77, wakati la Kagera Sugar limefungwa na kiungo Cleophace Anthony Mkandala dakika ya 90’+5.
Kwa ushindi huo, Tabora United imefikisha pointi 31, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi tatu na Singida Black Stars baada ya wote kucheza mechi 18.
Kwa upande wake Kagera Sugar hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo huo wakibaki na pointi zao 12 za mechi 18 Sasa nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment