WENYEJI, Tabora United wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kengold walianza kupata bao lilkfungwa kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji wake tegemeo, Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' dakika ya 25, kabla ya mshambuliaji Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo kuisawazishia Tabora United dakika ya 87.
Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi 32 na inabaki nafasi ya tano, nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi 37 baada ya wote kucheza mechi 19.
Kwa upande wao Kengold baada ya sare ya leo wanaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16 wakifikisha pointi 10 katika mchezo wa 19 pia.
0 comments:
Post a Comment