WENYEJI, Singida Black Stars imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Jonathan Sowah dakika ya saba na Marouf Tchakei dakika ya 62 kwa penalti, wakati ya Kagera Sugar yamefungwa na Salehe Kambenga dakika ya 21 na Halifa Hassan dakika ya 59.
Kwa matokeo hayo, Black Stars inafikisha pointi 34 na inabaki nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar inafikisha pointi 12 na inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 17.
0 comments:
Post a Comment