TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na washambuliaji, Mghana Jonathan Sowah mawili, dakika ya 57 kwa penalti na dakika ya 60, wakati lingine limefungwa na Mkenya Elvis Rupia dakika ya 90.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 41 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya nne, ikizidiwa pointi tatu na Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Mashujaa wanabaki na pointi zao 23 za mechi 22 pia na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 10.
0 comments:
Post a Comment