BAO pekee la mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 51 limeipa Singida Black Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa pointi mbili na Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Kwa upande wao JKT Tanzania baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 19 pia nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment