WENYEJI, Singida Black Stars wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na washambuliaji, Muivory Coast, N'guessan Serge Archange Pokou dakika ya 10 na Mghana, Jonathan Sowah kwa penalti dakika ya 32, wakati ya Pamba yote yamefungwa na mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 28 na 47.
Kwa matokeo hayo, Singida Black Stars inafikisha pointi 38 na inabaki nafasi ya nne, wakati Pamba inafikisha pointi 22 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 21.
0 comments:
Post a Comment