// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBA JIJI YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 KIRUMBA NA KUJITOA ‘DANGER ZONE’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBA JIJI YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 KIRUMBA NA KUJITOA ‘DANGER ZONE’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Saturday, February 15, 2025

    PAMBA JIJI YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 KIRUMBA NA KUJITOA ‘DANGER ZONE’


    WENYEJI, Pamba Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Mabao ya Pamba Jiji leo yamefungwa na kiungo John Ben Nakibinge dakika ya 18 na mshambuliaji Mguinea, Abdoulaye Yonta Camara dakika ya 21.
    Kwa ushindi huo, Pamba Jiji wanafikisha pointi 21 na kupanda kutoka nafasi ya 13 hadi ya nane ikizizidi tu wastani wa mabao Namungo FC na Fountain Gate baada ya wote kucheza mechi 19.
    Kwa upande wao Coastal Union baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 22 za mechi 19 pia wakibaki katika nafasi ya tisa, wakiizidi wastani wa mabao tu KMC ambayo nayo ina mechi 19 za kucheza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA JIJI YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 KIRUMBA NA KUJITOA ‘DANGER ZONE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry