BAO pekee la Ibrahim Joshua dakika ya tatu limeipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nane, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 17 nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 19.
0 comments:
Post a Comment