WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Pius Buswita dakika y 44 na Erasto Nyoni dakika ya 56 kwa penalti, wakati ya Dodoma Jiji yamefungwa na Paul Peter dakika ya 21 na Apollo Otieno dakika ya 31.
Kwa matokeo hayo, Namungo FC wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 18 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati Dodoma Jiji wanafikisha pointi 20 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nane.
0 comments:
Post a Comment