MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya Simba SC na Azam FC umehamishwa kutoka Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge hadi Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kesho.
Aidha, taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) pia imesema badala ya Saa 10:00 jioni, sasa mechi hiyo ya mahasimu wa Jiji itaanza Saa 1:00 usiku, sababu ya kubadili Uwanja ikiwa ni udogo wa KMC Complex ukilinganisha na ukubwa wa mechi yenyewe.
0 comments:
Post a Comment