WENYEJI, Mashujaa wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mabao ya Mashujaa FC leo yamefungwa na kiungo Hassan Haji Ali dakika ya 35 na winga David Richard Ulomi dakika ya 83 — na kwa ushindi huo, Mashujaa inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 20 na kuruka kutoka nafasi ya 13 hadi ya sita.
Kwa upande wao Pamba Jiji FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 20 pia na kushukia kwa nafasi moja hadi ya 12 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.
Timu nyingine mbili zitakazomaliza nafasi y 13 na 14 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment