WENYEJI, KMC wamebuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yaliyoizamisha Singida Black Stars leo yote yamefungwa na Paul Oscar dakika ya 35 na 40.
KMC inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 18 pia na kusogea nafasi ya tisa, wakati Singida Black Stars inabaki na pointi zake 34 nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 18 pia.
0 comments:
Post a Comment