BAO pekee la winga Iddi Kipagwile dakika ya 38 limeipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 20 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 22 za mechi 21 nafasi ya 11.
0 comments:
Post a Comment