WENYEJI, Kengold wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Bao pekee lililoipa pointi tatu muhimu Kengold inayopambana kwa bidi kuepuka kushuka daraja – limefungwa na kiungo Mishamo Daud Charles dakika ya 81 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji, Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi'.
Kwa ushindi huo, Kengold wanafikisha pointi 13, ingawa wanaendelea kushika mkia katika ligi ya timu ya 16, wakizidiwa pointi mbili na Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 20 sasa.
0 comments:
Post a Comment