// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KENGOLD YAICHAPA FOUNTAIN GATE MABAO 2-0 UWANJA WA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KENGOLD YAICHAPA FOUNTAIN GATE MABAO 2-0 UWANJA WA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Monday, February 10, 2025

    KENGOLD YAICHAPA FOUNTAIN GATE MABAO 2-0 UWANJA WA SOKOINE


    WENYEJI, Kengold wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.  
    Mabao ya Kengold yamefungwa na mshambuliaji Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' dakika ya 33 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Fadhil Kisungi na la pili amefunga mshambuliaji Mzambia, Obrey Choro Chirwa dakika ya 83 akimalizia pasi ya Rodgers Gabriel.
    Kwa ushindi huo, Kengold inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 18, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 21 za mechi 18 pia nafasi ya saba. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KENGOLD YAICHAPA FOUNTAIN GATE MABAO 2-0 UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry