WENYEJI, Kengold wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mshambuliaji wa kushoto, Osacl Paul Mwaigaga alianza kuifungia KMC dakika ya 41, kabla ya mshambuliaji Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' kuisawazishia Kengold kwa penalti dakika ya 69.
Kwa matokeo hayo, Kengold wanafikisha pointi 14, ingawa wanandelea kushika mkia wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 21.
Kwa upande wao KMC wanafikisha pointi 23 katika mechi ya 21 pia na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 10, wakizidiwa tu wastani wa mabao na Dodoma Jiji iliyocheza mechi 19, Coastal Union na Mashujaa zote mechi 20.
0 comments:
Post a Comment