WENYEJI, Pamba Jiji wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao lililowazamisha Azam FC leo limefungwa na kiungo mkongwe, Deus David Kaseke dakika ya 86, akigusa mpira wa kwanza baada tu ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya kiungo Mrundi, Shassir Nahimana.
Ushindi huo wa pili mfululizo wakitoka kushinda ugenini dhidi ya Dodoma Jiji 1-0 pia — unaifanya Pamba Jiji FC ifikishe pointi 18 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 12, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 39 za mechi 18 pia nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment