WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na mshambuliaji Mganda, Peter Lwasa mawili, dakika ya 23 na 34 yote kwa penalti na Saleh Seif dakika ya 90’+2.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 15, ingawa inabaki nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 na Fountain Gate inabaki na pointi zake 21 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 19.
0 comments:
Post a Comment