TIMU ya Kagera Sugar imeambulia sare ya mabao mbele ya wageni wao, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 16 na inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, wakati KMC inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 22.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi y 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment